LICHA ya kukaa kwenye ndoa zaidi ya miaka minne, Mke mkubwa wa mpiga picha wa msanii Diamond Platnumz, Ashraf Lukamba, ‘Lukamba’ anayejulikana kwa jina la Shuu Mimi, amepasua jipu kuwa hana uhusiano wowote na mpiga picha huyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Lukamba kuposti picha ya mke wake mdogo ‘Cecy’ katika akaunti yake ya Instagram na miongoni mwa wafuasi wake kwenye ukurasa huo, walitoa maoni kuhoji kwanini Lukamba alimposti mke mdogo tu na kumtema mke mkubwa
“Lukamba una ubaguzi sana, kwa nini hujamposti Shuu, watendee haki wote,” aliandika Pretty Naah. Aidha, kabla Lukamba hajajibu chochote, mke huyo mkubwa yaani Shuu Mimi alimjibu, “Usinitag page za watu.
Mimi na yeye hatuna uhusiano wowote ule, mwambieni tu awaeleze ukweli. Tangu kuolewa kwa mke mdogo, matukio mbalimbali yamekuwa yakitokea kwa mke mkubwa wa Lukamba, ambapo siku kadhaa zilizopita, aliburuzwa polisi na mke mdogo kwa tuhuma za kumtukana mtandaoni.