Mmea mkubwa unaokula nyama unajulikana kama 'Montane Pitche' wa aina ya 'Nepenthes Rajah' na una urefu wa sentimita 41
Ulionekana Kisiwa cha Borneo mwaka 2011. Mmea huu ambao una kama dibwi (Pitch) unatumia majimaji yake kuwavutia na kuwanasa wadudu warukao kama buibui wakati mwingine hukamata hata mijusi na vyura
Mimea mingine inayokula nyama ni Flypaper Plant, Cobra Lily na Venus Flytrap
Katika yote hiyo uliovunja rekodi ya kula viumbe wakubwa ni huo Nepenthes Rajah ambao umeingia kwenye Rekodi ya Dunia