Morrison Ngoma Ngumu Simba SC



KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ameonekana kuwa na maisha magumu ndani ya kikosi cha Simba, hii ni baada ya kutokuwa na uhakika wa kumaliza dakika tisini kama ilivyokuwa anaitumikia Yanga.

Morrison ambaye amejiunga na Simba msimu huu baada ya kumaliza mkataba wa miezi sita ndani ya Yanga, mpaka sasa amefanikiwa kucheza mechi tatu za kimashindano ndani ya kikosi hicho.

Katika mechi hizo, amefunga mabao bao moja na kutengenezea mabao mawili.Katika mechi hizo zote, Morrison hakutoboa dakika tisini na kushuhudia akiishia dakika 60 tu.

Katika mechi ya kwanza ya Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Morrison alitoka dakika ya 66 na kuingia Rally Bwalya. Simba ilishinda 2-0.

Mechi ya pili ilikuwa ni kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kumalizika kwa Simba kushinda 2-1. Morrison alitoka dakika ya 67, nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Ajibu.

Kiungo huyo aliyekuwa maarufu ndani ya Yanga kiasi cha kucheza muda mwingi kwenye mechi, wakati Simba ikitoka sare ya 1-1 na Mtibwa kwenye Ligi Kuu Bara mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, alitoka dakika ya 66, akaingia Meddie Kagere.

Kocha Sven amezungumzia hilo akisema: “Katika kikosi changu, kila mchezaji ana nafasi ya kucheza, nina kikosi kipana, hivyo nawapa nafasi wote kuona uwezo wao kabla ya kupata kikosi cha kwanza cha uhakika.”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad