KOCHA Mkuu wa Yanga Mserbia, Zlatko Krmpotic kwa mara ya kwanza juzi alimbadilishia majukumu kiungo wake fundi raia wa Angola, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ wakati timu hiyo ilipocheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Mlandege ya Zanzibar.
Yanga ilicheza mchezo huo juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Azam Complex, Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar katika kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara watakaocheza dhidi ya Kagera Sugar.
Timu hiyo itakipiga na Kagera kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa ambao Yanga wanahitaji pointi tatu ili wajiweke katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi
Mserbia huyo juzi kwa mara ya kwanza alimchezesha kiungo wa kutokea pembeni namba saba ambayo katika michezo miwili iliyopita ya ligi walikuwa wakicheza Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Ditram Nchimbi.
Kocha huyo katika michezo miwili iliyopita wa ligi na wa kirafiki wa Wiki ya Mwananchi alikuwa akimtumia staa mpya kucheza namba nane iliyokuwa ikichezwa na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ akitokea benchi.
Katika mchezo wa ligi alioanza kucheza Carlinhos ni dhidi ya Mbeya City baada ya kutoka kucheza wa kirafiki na Aigle Noir ya nchini Burundi ambayo yote alitokea benchi.
Kiungo huyo juzi katika mchezo dhidi ya Mlandege aliingia kuchukua nafasi ya Farid Mussa na kufanikiwa kupiga pasi 16 kati ya hizo zilizofika ni mbili pekee, faulo mbili, kona tatu, krosi nne huku akipiga faulo mbili pekee ndani ya dakika 45 alizocheza akitokea bench