Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema pamoja na benchi la ufundi kukaa na timu kwa takribani siku 20, mabadiliko ya kiuchezaji yameanza kuonekana.
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Yanga waliondoka na alama zote tatu kwa ushindi wa bao 1-0, Mwambusi amesema leo waliingia kimbinu zaidi kutokana na kufahamu mazingira ya uwanja sio rafiki.
Aidha Mwambusi amewataka mashabiki wasiwe na hofu kuhusu timu yao kwani wakati utafika wataanza kugawa dozi nene kwa wapinzani wao
"Kocha amekaa na timu siku 20, unaona kabisa timu inabadilika na inatengenezeka taratibu. Kuna muda tutaanza kutoa dozi goli 10 , 8 siku chache zijazo.
Alipoulizwa juu ya kwa nini walimtumia Carlinhos kuchezeshwa pembeni ya Uwanja , Mwambusi alisema"Kumtumia Carlinhos pembeni ilikuwa ni mbinu ya mchezo, ni mchezaji mzuri ambaye mipira yake huwa na madhara kwa wapinzani, hivyo tulilazimika kumweka pembeni ili apate nafasi ya kucheza bila kuzongwa.
Katika hatua nyingine Mwambusi aliongeza kuwa"Mapungufu ya jana tunaenda kuyafanyia kazi na tutarudi tukiwa bora zaidi mchezo ujao dhidi ya Coastal Union," amesema
Yanga imeshinda mechi zote mbili za ugenini, huku safu yao ya ulinzi ikiendelea kuwa imara kwa kutoruhusu nyavu zao kuguswa