Mwanadamu wa Kale Alioka Mikate Kabla ya Kuanza Kilimo....



Kikundi cha Wanaakiolojia kimesema wamegundua kwamba Binadamu walianza Kuoka Mikate ya Nafaka Pori mapema zaidi kabla ya kuanza shughuli za kilimo

Utafiti uliotolewa kwenye Jarida la PNAS la Marekani unaonesha kuwa Wanaakiolojia wamegundua Mabaki ya Mikate ya kuokwa yenye historia ya miaka 14,400 katika makazi ya kale ya binadamu Kaskazini Mashariki mwa Jordan

Watafiti kutoka wamegundua kuwa binadamu wa kale walisaga, kuchuja, kukaanga na kupika nafaka pori, zikiwemo Shayiri na Ngano

Wamesema kuoka mikate kwa nafaka pori kuliwahimiza binadamu wa kale kuanza kulima nafaka, na kuleta mapinduzi ya kilimo katika Zama za Mwisho za Mawe

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad