Mwanamke afariki dunia baada ya kuzini na shemeji yake Gesti



Polisi jijini Nairobi nchini Kenya, wanafanya uchunguzi wa mwanamke mmoja aitwaye Jesca Sibwe mwenye umri wa miaka 42, ambaye amefariki dunia baada ya kulala nyumba ya wageni (Gesti house), usiku kucha na shemeji yake aitwaye John Kisongona Mareko.


Kwa mujibu wa Tuko news, inasemekana marehemu Jesca Sibwe, ambaye anatoka Kasarani alianza kuugua ghafla kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta.


Ripoti ya polisi nchini Kenya inasema , Jesca alialikwa na ndugu wa kiume wa mumewe John Mareko kwenye hoteli ya Graceland maeneo ya Dubois siku ya Jumatano, Septemba 23,2020.


Mareko alikuwa amewasili saa moja kutoka Malindi ambapo wawili hao walilala katika hoteli ya Graceland.


Inaelezwa kuwa, Mwanamke huyo alianza kukohoa na ndipo wakaitisha teksi ya kumkimbiza KNH ambapo madaktari walithibistisha tayari alikuwa amekata roho


Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali hiyo kusubiri upasuaji huku maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wakianzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad