Mwanamke aliyejikata mkono wake akutwa na hatia ya utapeli


Mwanamke mmoja raia wa Slovenian amekutwa na hatia kwa baada ya kujikata kwa makusudi mkono wake mwenyewe kwa nia ya kulaghai kwenye bima.
Mahakama iliyopo mji mkuu wa Ljubljana umebaini kuwa Julija Adlesic, mwenye umri wa miaka 22, alikuwa ametoa sera tano za bima mwaka mmoja kabla hajapata jeraha.

Alidai kuwa alijikata wakati akikata tawi.

Adlesic alikuwa anataka kupata zaidi ya Euro milioni moja (, $1.16m) kwa ajili ya matibabu.

Kwa sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka miwili gerezani huku mpenzi wake alifungwa miaka mitatu.

Adlesic na baadhi ya ndugu zake walikamatwa mwaka 2019 baada ya kuwasili hospitalini huku mkono wake ukiwa umekatika.

Mahakama ilibaini kuwa mwanamke huyo na mpenzi wake walikusudia kuacha mkono uliokatika nyuma badala ya kwenda nao hospitalini ili kuhakikisha kuwa ulemavu huo unakuwa wa kudumu.

Ingawa mamlaka waliupata mkono huo kwa wakati na kuweza kumshonea.

Waendesha mashtaka wamesema mchumba wa mwanamke huyo alitafuta mtandaoni maelezo kuhusu mkono wa bandia siku moja kabla ya mkono wa mpenzi wake kukatika.

Waendesha mashtaka wanasema huo ni ushaidi kuwa jeraha lile lilipangwa kufanyika kwa makusudi.

Baba yake mpenzi wakeAdlesic alipewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja.

Wakati wa kusikiliza mashitaka, Adlesic alikanusha kudhamiria kujikata mkono wake.

Wapenzi hao walifanikiwa kufanya utapeli huo , na watapokea zaidi ya euro nusu milioni na malipo mengine watalipwa kila mwezi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad