Nimeleta mada hii tujadili tuone ni wapi mtu anapokuwa sahihi na wapi mtu anakosea.
Mkataba wa ndoa unawataka wanandoa kuvumiliana katika SHIDA na RAHA.
Sasa chukulia mmeoana halafu inafikia mahali maisha yanakuwa magumu hata milo miwili inashindikana, hivyo mwanamke anaamua kumkimbia mumewe.
Mwanaume anapobaki mwenyewe anaparangana japo maisha yanarudi kwenye mstari, na hapo mwanamke anaanza kutaka kurudi tena kwa nguvu kwakuwa bado ni mke halali.
Usahihi wa huyu mwanamke ni upi. Kabla hajaingia kwa nyumba, mwanaume alikuwa vizuri na pengine mwanamke alichangia ufukara katika familia hiyo kwani alipoondoka, mali zilirejea, na yeye akataka kurejea tena. Je kama wewe ndo mwanaume utampokea tena? Tuangalie pande zote.
Karibu tuchangie.
'Mkataba wa ndoa unawataka wanandoa kuvumiliana katika SHIDA na RAHA' nukuu hiyo sentensi hakuna ndoa wala mapenzi tena hapo
ReplyDeleteWewe mwandishi acha tu. Haya mambo ya Ndoa ni magumu sana. Hawa wanawake muwe mnawaangalia tu na kupishana nao. Sasa angalia unakuta mwanamke mzima yuko ndani ya ndoa lakini kisa tu kakorofishana kidogo na mme wake anakufuata wewe mwanaume na kukufungukia siri zote za jamaa yake. Na mchezo anakupatia vilevile. Mimi nakwambia haya mambo ya wanawake acha kabisa. Niseme ni kwa bahati mbaya sana niliwahi kuwamo ndani ya ndoa, lakini mambo hayakwenda vile ndivyo na sasa niko nje ya hiyo Ndoa. Nimebakia kama muangaliaji wa vile game inavyokwenda. Pamoja na hayo namshukuru mja wake. Maana ilikuwa balaaaa dah!!! Poleni sana wahanga wa hiyo game. Kwani sio mchezo.
ReplyDeleteUjue kitu chochote akifanya mwanamke huwa kinaonekana kikubwaaaa, lakini hiko hiko akifanya mwanaume anaonekana bora. Kuna wanaume wangapi hapa ni walevi, malaya, nk. unataka kuniambia sababu ni mwanamke hapana. wakati mwingine ni wewe mwenyewe. Wanaume wengi si wavumilivu lakini mnataka wanawake wawe wavumilivu. Kivipi, kwanini, ili iweje. IFIKIE HATUA TUJITAMBUE KILA MMOJA NA NAFASI YAKE NA SI KULAUMIANA NO HAISAIDII. ZAIDI UTAMKOSEA MUNGU WAKO UONEKANE UNA GUNDU. JILEKEBISHE WEWE KWANZA HARAFU LEKEBISHA WENZIO
ReplyDelete