Naibu mkuu wa jimbo auwawa nchini Afghanistan




Nchini Afghanistan, naibu mkuu wa jimbo la kusini la Paktiya, Ayub Gharwal ameuwawa leo na watu wenye kujihami na silaha ambao hawakuweza kufahamika. 

Taarifa kutoka katika mamlaka ya jimbo hilo zinasema Gharwal alivamiwa wakati akiwa njiani kulekea katika chuo kikuu cha mji mkuu wa jimbo wa Gardiz. 


Hata hivyo hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na tukio hilo, lakini kwa muda mrefu kundi la Taliban limekuwa na nguvu katika maeneo ya jimbo hilo.


 Wakati huohuo, Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani pamoja kuungana na familia ya Gharwal katika kuomboleza kifo hicho amesema wanamgambo wa Taliban wanapaswa kukubaliana na hamu ya Waafghanistan ya kusitishia mapigano. 


Kwa mara kadhaa kundi la Taliban limekuwa likikataa usitishwaji wowote wa mapigano, ingawa linashiriki pamoja na ujumbe wa upatanishi wa serikali ya Afghanistan, katika mazungumzo ya Doha, yenye lengo la kutafuta suluhisho la kisiasa kufuatia mgogoro unaendelea nchini mwao.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad