Msanii wa Bongofleva Caby Nedvarda amefunguka kuwa msanii Nandy hakuwahi kuwa mke mwenzake na hawezi kuwa mke mwenzake pia hapendi kumuongelea sana kwa sababu anahisi atampa promo ya bure.
Akizungmza na EATV & EA Radio Digital Caby Nedvarda amesema kuwa yeye ndiyo alianza kuwa na huyo mtu kwa miaka 10 iliyopita hivyo hawezi kuwa mke mwenzake.
"Kuhusu comments zinazoendelea kwa mimi na Nandy huwa hata sisomagi kwanza, hakuwahi kuwa mke mwenzangu na sidhani kama ni mke mwenzangu au aliwahi kuwa mke mwenzangu, japo linavyomzungumziwa naona kama ni maneno ya waja tu kwa sababu sio kama kila mtu atakupenda au kukufurahia, wakati wa mabaya unapokea na wakati wa mazuri unapokea pia"