Katibu mkuu wa jumuiya wa kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amaitaka Urusi ishirikiane kikamilifu na shirika la kupiga marufuku silaha za nyuklia katika kufanyika uchunguzi wa haki juu ya madai ya kupewa sumu kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny.
Stoltenberg amesema msimamo wa NATO juu ya kupewa sumu kiongozi huyo unatokana na sera ya kupinga matumizi haramu ya silaha za sumu ambazo zimepigwa marufuku kwa mujibu wa sheria na kanuni za kimataifa.
Naye Rais Donald Trump amesema Marekani haina ushahidi iwapo bwana Navalny alipewa sumu lakini ameleeza kuwa nchi yake haina sababu ya kutilia mashaka kilichobainishwa na Ujerumani.