"Natumaini CHADEMA wataniunga mkono"- Kubenea



Mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia ACT Wazalendo,  Saed Kubenea, amesema kuwa hata kama vyama vya upinzani vitaamua kuungana na kuachiana baadhi ya majimbo ya uchaguzi, anayo imani kuwa chama cha CHADEMA kitamuunga mkono na kuhakikisha anapata ushindi katika jimbo hilo



Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 26, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ambapo amesema kuwa licha ya kwamba amechelewa kuzindua rasmi kampeni zake kutokana na matatizo yanayomkabili, lakini kampeni zake atazindua rasmi siku ya kesho ya Septemba 27,




"Mimi ni mtiifu wa maelekezo na maamuzi ya chama changu na kama chama kitasema jimbo la Kinondoni anaachiwa CHADEMA basi mimi nitakubali kuachia hilo jimbo ili mgombea wa CHADEMA aweze kugombea, lakini mimi matumaini yangu kwa kuwa mgombea wa CHADEMA anaweza kupata Ubunge kupitia dirisha lingine la viti maalum, naamini CHADEMA wataniunga mkono mimi ili hatimaye Kinondoni iweze kuongozwa na mimi", amesema Kubenea.




Aidha kubenea ameeleza ni kwa namna gani kesi yake mahakamani imemrudisha nyuma, "Matatizo yamenirudisha nyuma sababu yamevuruga mipango niliyokuwa nayo, yamenifanya niwe 'busy' na kesi badala ya kufikiria uchaguzi, nimepoteza mawasiliano sababu simu yangu ipo polisi, lakini pia yameniimarisha sana na nipo imara bado".

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad