NBAA: Ni kosa kufanya kazi za kihasibu na kikaguzi bila kusajiliwa


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imesema kuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufanya kazi za kihasibu na kikaguzi bila kusajiliwa na Bodi hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam, Afisa Masoko na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Magreth Kageya amesema ni kosa kwa baadhi ya Vikundi, Taasisi kuajiri watu na kuwapa vyeo vya Uhasibu na Ukaguzi.

Kageya amesema hairuhusiwi watu kupewa vyeo hivyo bila kupita ngazi maalum katika Bodi hiyo sambamba na kufikia ngazi ya CPA, ameshauri Taasisi, Mashirika hayo kuuliza kwa Bodi hiyo ni mtu wa aina gani anapaswa kuwa Mhasibu au Mkaguzi.

Kwa upande wake, Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka amesema Bodi hiyo kwa sasa ina Kitengo cha (Member Service) ambapo chini yake kuna Audit Quality Review (AQR) ambayo inahusika kukagua kuhakikisha Kaguzi zinafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi na kukidhi viwango vya Kimataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad