Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yawaita viongozi wakuu vyama vyote



Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewaita viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa ili wazungumzie utekelezaji wa sheria zinazosimamiwa na ofisi hiyo.

Taarifa ya ofisi hyo kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye usajili wa kudumu, imeeleza kuwa kikao hicho cha


viongozi wakuu wa vyama na Msajili wa Vyama vya Siasa kitafanyika Oktoba 2, mwaka huu jijini DSM.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza kikao hicho kitaanza saa 2 asubuhi na


kwamba kitaanza mapema kwa kuwa Ijumaa ni siku ya ibada.




“Washiriki watakuwa ni Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu, mnaombwa kuhudhuria bila kukosa” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa kwa niaba ya Msajili wa Vyama Vya Siasa.




Hivi karibuni Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilikiandikia barua Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)


kuhusu kitendo cha kumnadi huko Zanzibar Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif wa


ACT-Wazalendo, kwani jambo hilo ni kinyume cha sheria.


Ofisi hiyo ilieleza kuwa kwa sasa hakuna chama chochote cha siasa, kinachoweza kushirikiana katika uchaguzi mkuu wa


mwaka huu ; na endapo kitafanya hivyo kitafanya kosa la kisheria.


Nyahoza alisema kutokana na kosa kama hilo, tayari ofisi ya msajili imekiandikia Chadema barua ya kukitaka kujieleza kwa


kitendo chake cha kumnadi Maalim Seif huko Zanzibar na pia kumnadi Zitto huko Kigoma.


“Tunataka wajieleze huo ushirikiano ukoje na ACT?” alisema kwa mujibu wa sheria, vyama hivyo kama vilitaka kushirikiana vilitakiwa kufuata utaratibu kabla ya uchaguzi, kwa maana ya kufanya mkutano wa makubaliano, waingie mkataba wa makubaliano na kuukabidhi mkataba huo wa makubaliano kwa msajili miezi mitatu kabla ya uchaguzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad