Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Morogoro limefanikiwa kuudhibiti moto wa mafuta kutokana na gari lenye namba za usajili T862 BZS na tela namba T814 DBZ kushika moto katika eneo la Kiegea, Wilayani Kilosa.
Gari hilo mali ya kampuni ya INTERPETROL lililokuwa limepakia shehena kubwa ya mafuta aina ya dizeli lilikuwa likielekea nchini Burundi kutokea Jijini Dar es Salaam likiwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Issa raia wa Burundi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF), Goodluck Zelote amesema hakukuwa na madhara yoyote kwa binadamu na chanzo cha moto huo hakikujulikana mara moja ila inasadikika ni hitilafu katika mfumo wa umeme wa gari hilo.