Rais wa Zambia Edgar Lungu, aongoza nchi kuomboleza kifo cha samaki ‘Mafishi’



Zambia inaomboleza kifo cha samaki wake mkubwa katika chuo kikuu cha umma cha Copperbelt (CBU). Samaki huyo aliyejulikana kama Mafishi – ameombolezwa na rais Edgar Lungu na kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema.




Neno Mafishi limekuwa likisambaa kwa kasi katika mtandao wa Twitter nchini Zambia kufuatia kifo cha samaki huyo Jumatatu usiku.


Samaki huyo alikuwa akiishi katika kidimbwi cha chuo kikuu na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakimtembelea kabla ya kufanya mtihani ili kuomba wapite.


Wanafunzi wengine wanasema aliwasaidia kujiondolea msongo wa mawazo .


Rais Lungu alitumia nukuu ya Mahatma Gandhi kumuomboleza samaki huyo kwa kuandika:”ukuu wa taifa na maendeleo ya maadili yake yanaweza kuhukumiwa kutokana na jinsi anavyowatendea wanyama wake.”


Social embed from facebook

RipotiReport this social embed, make a complaint


Bwana Hichilema aliandika: “Tunaungana na jamii ya wanafunzi wa sasa na wazamani wa chuo kikuu cha CBU, kufuatia kifo chasamaki wao Mafishi.”


Samaki huyo alikuwa sehemu ya mpango wa turathi ya viumbe wa majini na anasemekana ameishi ndani ya kidimbwi cha chuo hicho kwa karibu miaka saba, kwa mujibu wa kituo cha kibinafsi cha televisheni, Diamond.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad