Salim Kikeke "Wanaosema Naihujumu Tanzania, Mungu Atawalipa"



MTANGAZAJI wa Shirika la Habari la Uingereza, BBC, Salim Kikeke, ambaye ni raia wa Tanzania ameonyesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watu aliodai kuwa wanamchafua wakisema anaihujumu na kuidharau Tanzania kwa kutoa habari zinazoididimiza Tanzania.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Kikeke ameamua kuvunja ukimya na kuandika haya:

“Nimesikitishwa sana na tuhuma zinazosambazwa mitandaoni dhidi yangu. Nataka kusema bayana kama Mtanzania, nawaheshimu watu wote nje na ndani ya Tanzania bila kujali jinsia umri au itikadi zao.


“Nimefanya kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 20 na kamwe sijawahi na sitowahi kufanya kitendo chochote cha kuhujumu, kutukana au kudharau mtu au nchi yoyote ikiwemo Tanzania na wananchi wake.
“Wanaosambaza uzushi juu yangu wana lengo la kuchafua sifa na jina langu ambalo nimejenga kwa kujituma na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili.


“Maelfu ya vijana duniani wamehamasika kutokana na bidii na historia yangu. Waswahili wanasema mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe, mimi sina kinyongo na wanaotaka kunidhalilisha, kwa imani yangu Mwenyezi Mungu atawapa wanachostahili. Shukran,” amesema Kikeke.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad