Salum Mwalimu atoa ahadi ya CHADEMA kwa watumishi


Katika muendelezo wa kampeni za Urais za CHADEMA, mgombea mwenza Salum Mwalimu amesema kuwa chama hicho kikiingia madarakani kitalipa fidia ya nyongeza ya mishara ya watumishi wa serikali ambao hawakupata kwa muda wa miaka mitano kwa mujibu wa sheria.
Salum Mwalimu amesema hayo wakati  akinadi sera za chama hicho katika mkoa wa Kilimanjaro leo Septemba 12, 2020 ambapo pamoja na mambo mengine amejinadi kuwa atahakikisha kila Mtanzania anapata bima ya afya kwa kuwa haki hiyo ni ya msingi na kwamba ili taifa liwe na maendeleo lazima watu wake wawe na afya njema.

"Watumishi wote walio chini ya Serikali tutakwenda kuwalipa  fidia ya nyongeza ya mishahara yao ya miaka mitano waliostahili kwa mujibu wa sheria", amesema Salum Mwalimu.

"Tunakwenda kuhakikisha kila mtanzania anapata bima ya afya, ukijua kuwa wewe ni Mtanzania lazima uwe na bima ya afya, bima ya afya ni haki ya msingi", ameongeza.

Aidha mgombea mwenza huyo amewataka vijana kufanya maamuzi sahihi ili kuhakikisha wanapata mtetezi ambae atazingatia maslai yao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad