Mshambuliaji wa timu ya soka nchini Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkataba wa miaka minne kutoka Aston Villa.
Klabu hiyo imeandika katika mtandao wake kwamba imemuongeza nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania katika kikosi chake kwa mkataba wa miaka minne
Mchezaji huyo aliyeshinda taji la mfungaji bora mara kadhaa nchini Ubelgiji kabla ya kujiunga na Aston Villa nchini Uingereza atahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja kabla ya kuandikisha kandarasi ya kudumu ya miaka minne.