Samatta Asepa na Kijiji Chake Villa, Kuvuna Sh16 Milioni kwa Siku



NAHODHA wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesepa na kijiji huko Aston Villa baada ya kukamilisha dili lake la uhamisho wa mkopo wa kutua Fenerbahce huku mashabiki wakimwambia “Ulipo tupo Poppa.”


Samatta ametua katika klabu hiyo ya Uturuki kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu huu, huku akiingia maafikiano ya kusajili mkataba wa miaka minne baada ya muda huo wa mkopo kumalizikia.


Wafuasi wa mshambuliaji huyo walikuwa katika kampeni nzito ya ku-unfollow ukurasa wa Instagram wa Aston Villa mara baada ya Samatta kutambulishwa katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uturuki.



 

Mastaa wakubwa wa fani mbalimbali nchini na mashabiki wengine walionyesha sapoti kwa nahodha wao wa timu ya taifa kwa kutuma meseji mbalimbali za kumpa matumaini asikate tamaa, huku wengine wakijibizana na mashabiki wa Villa wakiwaambia waanamini kwamba mara hii timu yao haitanusurika kushuka daraja baada ya msimu uliopita kuponea tundu la sindano.


Samatta hajatua kinyonge huko Fenerbahce, ambako atalipwa mshahara wa zaidi ya Sh 116 milioni kwa wiki.


Tafsiri yake ni kwamba kwa kila siku ya Mungu hata kama atakuwa amelala ndani anaangalia katuni na wanaye Mil. 16 zinaingia kwenye akaunti yake. Achana na posho nyingine.


Klabu hiyo ya Uturuki imeafiki kulipa kitita cha Euro 6.5 milioni ( Sh 17.6 bilioni) kwa Villa ili ipate huduma ya mshambuliaji huyo wa Mbagala baada ya muda wake wa mkopo.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao mmoja wa wachambuzi wa Uturuki, Fenerbahce na Samatta zimekubaliana kuwa mshambuliaji huyo atalipwa kitita cha takribani Euro 2.25 milioni (Sh 6 bilioni) kwa mwaka.


Kiasi hicho cha fedha ukikigawa kwa wiki, ni takribani kiasi cha Euro 43,000 (Sh 116 milioni).


Kwa maana hiyo, kwa muda wa miaka minne ya mkataba wake na Fenerbahce, Samatta mwenye umri wa miaka 27, atapata mshahara wa jumla wa Euro 9 milioni (Sh 24 bilioni) ingawa pia atavuna fedha nyingine kupitia posho na bonasi kulingana na ufanisi wake na mafanikio ya timu kwa kipindi hicho atakachoichezea.


Fenerbahce italipa kumsajili Samatta kwa ada hiyo ya Euro 6.5 milioni (Sh 17.6 bilioni) ikiwa ataifungia zaidi ya mabao 15 katika kipindi cha mwaka mmoja atakayoichezea.


Ikumbukwe kwamba, mwezi Januari, Aston Villa ilimsajili Samatta kutokea KRC Genk kwa kitita cha Euro 9.5 milioni (Sh 25.6 bilioni).


Tangu ametua Villa, Samatta ameicheza mechi 16 na kuifungia mabao 2 katika michuano mbalimbali.



 



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad