Samatta Asepa, Watanzania Waiporomosha Ghafla Aston Villa



BAADHI  ya mashabiki wa soka wameamua ku-unfollow mtandao wa Instagram wa Aston Villa ghafla huku wengine wakiendelea kufanya hivyo kadiri muda unavyozidi kwenda.

Kitendo hicho cha mashabiki kujiondoa katika mtandao huo wa kijamii wa Aston Villa kimekuja mara tu baada ya mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta, kutangazwa kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.

Idadi ya wafuasi wa Instagram ya Aston Villa ilikuwa 915K hii ni kabla ya klabu hiyo kuweka wazi kuondoka kwa nyota huyo

Lakini mara baada ya kutangaza rasmi kuwa Samatta amejiunga na Fenerbahce wamemtakia kila la heri  na ndipo idadi ya wafuasi (followers)  ikaanza kushuka hadi kufikia 911K.

Mpaka sasa  followers wa Instagram wa Aston Villa wameshuka hadi kufikia 879K.

Kitendo kama hiki cha wafuasi kushuka katika klabu pindi mchezaji fulani anapoondoka au kuuzwa kilishawahi kutokea kwa mchezaji bora  duniani, Cristiano Ronaldo, alipotoka Real Madrid na kujiunga na Juventus.


Juventus ilifanikiwa kupata wafuasi milioni 4.7 baada ya kumsajili Cristiano Ronaldo wakati ndani ya saa 24 pekee Real Madrid iliwapoteza milioni moja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad