Senzo hajarudisha kadi ya Simba, majina ya Wadhamini wa klabu haya -Magori



Aliyekuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC na ambaye ni mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’,bwana Crescentius Magori amesema kuwa Senzo Mazingiza hajarudisha kadi mpaka sasa.


MAX SPORTS: SIMBA SPORTS CLUB: SENZO MAZINGIZA NDIE KIONGOZI MPYA SIMBA


Magori ambaye alimuachia nafasi ya CEO, Senzo Mazingiza ameyasema hayo kupitia kipindi cha michezo cha Efm Radio.


Akiulizwa kama kuna ubaya kumchagua mtu ambaye alikuwa mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ndiyo awe CEO, Magori amesema ”Wanaweza kuchagua, lakini tayari ameshaguliwa mjumbe huyo na ameshapitishwa kuwa CEO.”




Akijibu kama kitendo hiko hakitakuwa na mgongano wa kimaslahi Mgori amesema ”Hakuna mgongano wa maslahi, kwanza hapo tuna uhakika hatakimbilia timu nyingine, kwasababu ni mwanachama wa klabu hii, tumempata mwanachama mwenzetu ambaye anakuwa CEO, tofauti na kuwa mtu mwingine ambaye amekuja tu ambaye anaweza akafikiri hii ni kazi anabadilisha tu anakwenda upande mwingine.”


benkibilastress Instagram posts - Gramho.com


Akijibu swali kama kikatiba CEO anatakiwa kuwa mwanachama wa Simba, Crescentius Magori amesema ”Haitakiwi awe mwanachama,” alipoulizwa kama mtu anaweza kuja Simba kikazi na akawa mwanachchama amesema ndiyo ”Yes, na hata Senzo alichukua kadi ile, ndiyo alichukua kadi,” alipoulizwa kama aliirudisha Magori amesema ”Sijui rabda, sababu ni kadi ya benk anaweza akawa anatumia mpaka leo, alichukua kadi anayo, ile kadi ya Equity ile.”


Crescentius Magori amefafanua sababu za CEO sio lazima kuwa mwanachama wa Simba na kudai kuwa ni kazi ya utaalamu hivyo hawakutaka kujifunga katika katiba na kutolea mfano unaweza kumchukua mtu kutoka Benki Kuu lakini asiwe mwanachama wa Simba.

Magori amewataja pia wadhamani wa klabu hiyo ya Simba ambao ni, Mzee  Ramesh Patel, Adam Idd Mgoyi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Profesa juma kapuya na Mzee Abdul Wahid.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad