Tukio la kuhama kwa wanyama kati ya mbuga za wanyama za Kenya na Tanzania ni maarufu sanaImage caption: Tukio la kuhama kwa wanyama kati ya mbuga za wanyama za Kenya na Tanzania ni maarufu sana
Nchini Kenya maafisa wameifunga hoteli ya kifahari iliyojengwa katika mbuga ya wanyama , ambayoilionekana kufunga mapito ya wanyama wanaohama katika hifadhi ya wanyama maarufu ya Maasai Mara Game wiki iliyopita.
Tukio la kuhama kwa wanyama wa mbugani kati ya mbuga za wanyama za Maasai mara nchini Kenya na Serengeti nchini Tanzania ambalo hutokea kila mwaka katika eneo hilo ni maarufu sana na watalii wengi huja kulishuhudia kila mwaka.
Wiki iliyopita video ilionesha wanyama wakiwa wamekwama katika mto, huku hoteli hiyo ikiwa imefunga njia yao, na wafanyakazi wa hoteli wakiwafukuza wanyama, iliibua hasira miongoni mwa Wakenya hususan mitandaoni wakiitaka serikali ichukua hatua na sasa waziri wa utalii ameagiza ifungwe.
Wanyama hao huhama kila mwaka kwa ajili ya kutafuta malisho na kuzaliana.