Ofisi ya Rais – TAMISEMI imekanusha taarifa iliyotolewa na Mgombea Urais kupitia CHADEMA kwa kusema kuwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri nchi nzima wameitwa jijini Dodoma na Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli
Taarifa iliyotolewa imesema, Ofisi ya TAMISEMI ndiyo inayosimamia Watendaji wote Nchini na tuhuma alizozitoa Lissu ni za Uongo na Wananchi wote wanapaswa kuzipuuza kwasababu hazina ukweli wowote. Watendaji wote wapo katika vituo vyao vya kazi
Lissu alisema Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ndio Wasimamizi wa Uchaguzi hivyo kitendo cha kuitwa na Dkt. Magufuli kimempa wasiwasi kwamba wanakwenda kupewa maelekezo ambayo yanaweza kuleta matokeo yaliyotokea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi, Joseph Nyamhanga akizungumzia taarifa iliyotolewa na Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema kuhusu wakurugenzi wa halmashauri zote kuitwa Dodoma.