Serikali imetoa rambirambi ya Tsh. 250,000 kwa kila familia iliyofiwa na mtoto kwenye ajali ya moto katika Shule ya Msingi Islamic Byamungu, Kyerwa Mkoani Kagera
Aidha, Serikali inawagharamia wanafunzi wengine sita wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Bugando
Shule hiyo iliungua mabweni na kusababisha vifo vya watoto 10 na wengine 6 wakiwa wamejeruhiwa. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 9, usiku wa kuamkia Septemba 14
Watoto waliopoteza maisha wana umri wa miaka kati ya 6 hadi 12 na Jeshi la Zimamoto lilitoa wito kwa Shule kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika mazingira ya shule