Shigongo: Nimeacha Kila Kitu Niteseke Sababu ya Wana-Buchosa



MBOMBEA ubunge Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, amesema kuwa ameacha kila kitu alicho nacho ili kujitesa na kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo chanya katika jimbo hilo.


 


Kauli hiyo ameitoa jana, Ijumaa, Septemba 25, 2020, kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni Jimbo la Buchosa uliofanyika katika viwanja vya mpira Nyakaliro, Halmashauri ya Buchosa, Sengerema.


 


Akizungumza na wananchi hao, Shigongo alisema atatumia maarifa yake ambayo amekuwa akiyatumia kufundisha maelfu ya watu takribani nchi nzima, namna ya kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi.


 


“Ni muda sasa umefika tushirikiane ili jimbo letu lipate maendeleo kwani wananchi wanatamani kupata maendeleo kutoka kwetu,” alisema Shigongo.




Katika uzinduzi huo, Shigongo alisema atahakikisha anaboresha miundombinu ya elimu mashuleni ili watoto wapate elimu bora kama wanavyopata watoto wengine kwa kushirikiana na wananchi.


 


“Katika kuboresha elimu mkinichagua nitahakikisha walimu wanapata motisha pamoja na wanafunzi wanaofanya vizuri.  Kuwapatia zawadi hii itasaidia ufaulu kupanda katika shule zetu za msingi na sekondari,” alisisitiza.


 


Sambamba na elimu pia alisema ataboresha huduma ya afya, miundombinu ya barabara ili wananchi wa jimbo hilo wapate huduma bora  na kusafiri kwa urahisi katika maji na nchi kavu.


 


Aidha, katika sekta ya kilimo na uvuvi alisema kwenye uongozi wake, endapo atachaguliwa, atahakikisha wananchi wa  wanalima kilimo cha kisasa  na kuweka ulinzi madhubuti kwa wavuvi ili kupambana na maharamia wanaowadhuru  katika Ziwa Victoria ili  wanufaike na kuondokana na umasikini.


 


Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema, Marco Makoye, aliwataka wana-Buchosa na Sengerema kwa jumla wawapagie kura wagombea ubunge wa majimbo ya Sengerema na Buchosa  na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kuleta maendeleo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad