UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo mbele ya Gwambina FC itatoa burudani na kuwapa furaha mashabiki watakaojitokeza Uwanja wa Mkapa.
Septemba 26, Simba itakuwa na mchezo dhidi ya Gwambina FC ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuhitaji kupata pointi tatu muhimu.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanahitaji kutoa burudani na kupata pointi tatu ndani ya uwanja.
"Tunahitaji kutoa burudani na kufanya vizuri kwenye mchezo wetu ambao tutaingia uwanjani tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tunahitaji pointi tatu.
"Viingilio ni vilevile vyenye ladha ileile 3,000 mzunguko ni kero kwenda mbele, sambusa za kwenda mbele wamesema wameongeza wachezaji kitu kingine wameahidi kuonyesha ushindani mkubwa, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.
Simba inashuka uwanjani ikiwa imeshinda mechi mbili mbele ya Ihefu FC kwa ushindi wa mabao 2-1 na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United, sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar.
Gwambina FC imepoteza mechi mbili ikiwa ni ile ya ufunguzi dhidi ya Biashara United ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0,ilifungwa pia na Ruvu Shooting bao 1-0 na mechi yake ya sare ilikuwa mbele ya Kagera Sugar, ilikuwa ni sare ya bila kufungana.