SIMBA SC YAPATA MTENDAJI MKUU WA KWANZA MWANAMKE




Klabu ya Simba leo imemtambulisha Mwanadada Barbara Gonzalez kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu (CEO) ambaye anarithi mikoba ya aliyekuwa CEO Senzo Mbatha Mazingisa aliyetimkia Yanga SC.



Barbara anakuwa CEO mpya wa Simba SC baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Mohammed Dewji kukaa kikao chake hapo jana.


Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mo Dewji amesema kuwa sio yeye peke amemteua Barbara kushika nafasi hiyo, bali Mkutano wa Wajumbe wa Bodi ndio umempendeza baada ya kukaimu nafasi hiyo tangu kuachwa na Senzo.


Mo Dewji amemkaribisha klabuni hapo Barbara na kumwambia kuwa mvumilivu kutokana na mambo mbalimbali ambayo ni mazuri na mengine ya ovyo.


Pia amemtaka kupambana, kuendeleza farsafa ya Klabu hiyo iliyonayo hivi sasa.


Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez amewashukuru Wanasimba, Bodi ya Wakurugenzi, Mwenyekiti Mohammed Dewji kutokana na kufanya kazi pamoja karibu miaka mitatu katika mabadiliko ya mpito wa uwekezaji klabuni hapo.


"Tangu kuondoka Senzo Mbatha ni mwezi sasa, nimeshika nafasi kwa kukaimu kama Afisa Mtendaji Mkuu, kwa kweli tumepambana, 


"Niko hapa kuendeleza 'vision' ya Simba SC kwa upande wa Menejimenti, mimi nimenyooka na tutanyooka mbele, tumejipanga kwa ufupi", amesema Barbara.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad