Solksjear awapiga mkwara wachezaji wake



Kocha mkuu wa mashetani wekundu, Manchester united, Ole Gunnar Solskjaer amewataka wachezaji ambao hawapati nafasi katika kikosi cha kwanza waendelee kujituma mazoezini ili wamshawishi aweze kuwatumia katika michezo ijayo.

Solskjaer amesema kama miongoni mwao watabweteka hatowatumia hata kama wanachukizwa na jambo hilo kwasababu yeye kazi yake ni kufundisha mpira na sio kuwafanya wachezaji wawe na furaha.


"Wachezaji huwa wana furaha kama wanacheza vizuri na wanaopata ushindi katika mechi, lakini pia sio kazi yangu kuwafanya wawe na furaha mana kazi yangu ni kuchagua wachezaji bora ili waweze kunipatia matokeo bora" Alisema Solskjaer .


“ Ni kazi yao sasa kufanya mazoezi kwa bidii ili waendelee kuwa bora,na wakishafanya hivyo wasubrie kuchaguliwa sasa."


Miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Mnorway huyo ni mshambuliaji wa kiingereza,Jesse Lingard, ambaye hakucheza mechi ya kwanza ya ligi kuu msimu huu dhidi ya Crystal Palace, ambapo taarifa zinaeleza kuwa huenda akaondoka Old Trafford kwasababu mawakala wake tayari wanafanya mazungumzo na vilabu kadhaa nchini England na sehemu zingine barani ulaya


Wengine ambao rungu la kocha huyo limewadondokea ni Mlinda mlango, Sergio Romero,walinzi Chris Smalling, Phil Jones, Marcos Rojo na Andreas Pereira ambao na hawakuwepo katika mchezo wa kombe la Carabao dhidi ya Luton.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad