Soma Mkasa Huu: Walionicheka na kunidharau Wakati wa Matatizo, Wamenuna




Kuishi na binadamu yataka moyo na uvumilivu wa hali ya juu sana. Mimi ni mtumishi wa serikali na kijana ambaye sina muda mrefu Sana kazini. Mwanzoni nilikuwa na maisha mazuri ya wastani nikiwa na uwezo wa kuhudumia watoto wangu wawili na mke wangu ambaye naye kasoma lakini bado hajaajiriwa. Si mnajua baba makubwa hana mpango na ajira mpaka kila mtanzania awe na ndege yake mwenyewe na ikiwezekana na uwanja wa ndege. Hapa tutumie plan B.

Nje ya kusaidia familia yangu, sikuwaacha wazazi wangu, ndugu jamaa na marafiki kwa chochote pale nafasi iliporuhusu. Kwa kifupi nilikuwa kamtu fulani na kaheshima changu kwa ndugu jamaa na marafiki.


MATATIZO YANAANZA

Mwaka niilifukuzwa kazi katika mazingira ya kutatanisha/ ya uonevu. Nilipewa nafasi ya kukata rufaa na nilifanya hivyo kwa mamlaka za juu kwa mwenendo wa kesi hiyo nilijua nashinda lakini ni kwa muda gani? Pia nilijua nitapata kazi YOYOTE lakini halali, nasizitiza YOYOTE. Kwa vile sikujipanga kwa hili niliumia sana nilipowaangalia watoto wangu na mke wangu nililia Sana, sikujua kesho yetu ingekuaje. Mtoto wa kwanza yuko shule ya msingi private, ada hakuna, akarudishwa nyumbani.


MAUMIVU YANAZIDI

Baada ya kufuzwa kazi nilikaa wiki mbili bila kumwambia yeyote, hata mke wangu. Nikawa na msingi wa mawazo balaa baadae mke wangu alijua nina shida akaniuliza ikabidi nimwambie ukweli. ULICHEKA!!!!!!.Hapo nilikasirika na kuumia zaidi, baadae akaniambia usiwaze mume wangu hatujawa vilema, mbona watu weeengi hawajaajiriwa na maisha yanaendelea.


Badae kabisa nikaona haina haja kuficha kwani sijaua. Baada ya watu kujua sina kazi, wengine walifurahi sana wakisema tutakuwa wote mtaani. Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wakawa hawapokei simu zangu kabisa. Mara nyingine nakosa hata Mia watoto walia na njaa namwomba mtu wa karibu nisaidie hata elfu tano tu, anaanza kukupa mambo maendeleo yake na kuishia kusema, kwa sasa sina kabisa mpaka mwezi ujao na ukizingatia hapo ni terehe 8 ya mwezi. Mwezi ujao anakuweka blacklist, achaaaa bwana! Kila aliyeshiba amkumbuke mwenye njaa.


Siku moja nikaumia zaidi, jirani mmoja akawa anawaambia watoto wangu, nguo zimepauka jamani, hivi leo mmekula kweli? Sijakaa vizuri nikazipata kutoka kwa ndugu zangu wa damu kabisa wakisema kaka yetu amepotea kwenye ramani arudi kijijini tuu! Hawa ni watu ambao kufika walipo wametumia hela yangu ya kutosha tu. Mwanaume nikapiga kimyaaaa!

Nikarudia kusema nafanya kazi yoyote halali ili watoto wangu wasilale njaa. Hodi mtaani, zege liko wapi? Piga sana zege na zingine Kama hizo. Watoto wakawa wanapata chochote huku mke wangu naye akawa anapambana na vikazi vya hapa pale. Majirani wanatucheka ni dharau za wazi wazi lakini wanashangaa hatuwaombi chakula. Nikawa napigiwa simu na jamaa zangu wa mtaani, twende kuna kazi mahali, naenda tu.

Kuna siku tulienda kufanya kazi saiti, mwenye saiti akaja akaniita jina langu na kuniuliza kulikoni unafanya kazi hizi? Nikamwambia ukweli yaliyonisibu, alisikitika sana, achana na hii kazi akanipa laki 2 cash. Akanipeleka sokoni akanifanyia shopping ya vyakula vya kutosha, sikuamini. Akaniniambia ukiwa na shida niambie. Huyu ni mtu ambaye niliwahi kuhudumia vizuri nikiwa kazi kumbe hakunisahau. Wale jamaa ambao nilikuwa naenda nao saiti kunichukia wakisema, huyu sio mwenzetu, binadamu bwana achaa tu.

NAFANIKIWA

Mwezi uliopita nikapigiwa simu kazini nikachukue barua yangu, nikaenda. Kuisoma nikaambiwa unatakiwa kurudi kazini na ulipwe haki zako zote, nilifurahi Sana. Nikamushukuru Mungu. Sasa hivi nimeshaanza kwenda kazini tena ndugu zangu.

KAZINI SASA

Walionifanyia fitina wako matatani, wananionea aibu na wanaweweseka. Mungu awasamehe sina shida nao.

NDUGU JAMAA NA MARAFIKI

Wale wote walionicheka na kunidharau, sasa hivi wameninunia, waliokuwa hawapokei simu zangu, sasa hivi wananipigia. Sina shida nao, waniache nipambane na familia yangu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad