Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mtwara imefanikiwa kurejesha Zaidi ya Milioni Mia tano (536,956,762.28) zilizofanyiwa ubadhilifu wakati wa malipo ya zao la korosho msimu wa 2018/2019.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Takukuru Mkoani Mtwara ENOCK NGAILO amesema kuwa fedha hizo zilifanywa ubadhilifu na baadhi ya watu ambao sio waaminifu wakati wa malipo ya zao la korosho msimu wa 208/2019
Uchunguzi uliofanywa na Taasisi hiyo ya TAKUKURU uliwabaini badhi ya watumishi wa Serikali ambao walipewa jukumu la kuwa kweye timu ya uhakiki malipo ya zao hilo msimu wa 2018/2019 ambapo fedha hizo zililipwa na Serikali.
Aidha Takukuru Mkoani Mtwara ilifanya uchunguzi huo wa ubadhilifu wa fedha kwa kushirikiana na bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko Tanzania (CBT) iliyokuwa na jukumu la kusimamia malipo hayo..
Katika uchunguzi huo Taasisi hiyo ilibaini kiasi cha fedha cha shilingi 922,702,132.65 zililipwa kwa watu ambao hawakuuza korosho ,huku kiasi cha fedha cha shilingi 533,809,490.0. zililipwa kwa kuwazidishia wakulima waliouza korosho.
Hivyo kwa msimu wa mwaka 2018/19 jumla ya fedha shilingi 1,456,511,622.67 zililipwa kwa watu wasiohusika.
TAKUKURU Mkoani Mtwara imetoa wito kwa maafisa ushirika wa ngazi zote,wadau na Bodi za mazao mchanganyiko kila mmoja kusimamia Sheria na kanuni ili kuhakikish ushirika unajengwa katika misingi ili kuweza kuatatua matatizo na kupambana na Rushwa..