TAKUKURU: Ubwabwa Kwenye Kampeni ni Rushwa



Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amemuonya Hashim Rungwe ambaye ni mgombea Urais kupitia CHAUMMA kuwa kugawa chakula ‘ubwabwa’ wakati wa kampeni ni rushwa na ni kosa kisheria.

Myava alisema Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inapiga marufuku kwa mgombea kutoa vitu kama chakula kushawishi wapigakura ili wamchague. Rungwe amekuwa akiwaalika wafuasi wajae kwenye kampeni zake ikiwemo uzinduzi utakaofanyika Manzese, Dar es Salaam leo Septemba 5 kwa kuahidi ubwabwa utakuwepo.


Myava amesema kipindi hiki kinachotakiwa ni kunadi sera ili kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua na si kushawishi kwa kutoa rushwa.


Rungwe amesema atatumia ubwabwa kama CCM wanavyotumia wasanii, amesema kufanya hivyo si rushwa na amewataka wajiandae kupelekana mahakamani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad