YACOUBE Sogne, nyota mpya wa Yanga ambaye alitua nchini Tanzania Agosti 31 akitokea Burkina Faso na kupokelewa na viongozi wa Yanga takwimu zake zinaonyesha kuwa ni mtu kwelikweli.
Yanga wamemsajili mchezaji huyo akiwa ni wa mwisho kabisa kwenye usajili huu mkubwa, ukiwa ni muda mfupi kabla dirisha halijafungwa.
Akiwa ndani ya Asante Kotoko ya Ghana, Sogne alicheza jumla ya mechi 26, ambazo ni sawa na dakika 2,340 alipachika mabao sita, na kutoa jumla ya pasi tatu za mabao akiwa na wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 260.
Mshambuliaji huyo mwenye rasta kichwani aliwasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na mamia ya mashabiki ambao walijitokeza na timu ya Championi pia iliweka kambi hapo ambapo aliongea kwa kusema:“Ninawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kunipokea na ninaahidi kufanya kazi kweli,”.
Tayari nyota huyo amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na nyota wa zamani wa timu hiyo, Tariq Seif ambaye mkataba wake uliisha na Yanga haikuwa na mpango naye.