TANZIA: Baba wa bilionea Bill Gates afariki dunia



William Henry Gates II ambaye ni baba mzazi wa Bill Gates (mvumbuzi wa Microsoft )amefariki dunia siku ya Jumatatu Septemba 14, 2020 akiwa na umri wa miaka 94.


“Sote tumekuwa na muda mrefu kutafakari juu ya jinsi gani tulivyo na bahati ya kuwa na mtu huyu wa kushangaza maishani mwetu kwa miaka mingi,” ameandika Bill Gates


William Gates Sr. Dies at 94 | Hamodia.com


Mzee Gates alikuwa mwanajeshi mstaafu na mwanzilishi mshiriki wa ‘Seattle law firm’ hii ni kwa mujibu wa wasifu wake. Bill Gates amesema kuwa baba yake alikuwa na mchango mkubwa kwenye ushauri wa uanzilishi wa shirika la misaada ambalo limekuwa lengo kuu la Gates tangu alipoacha kuendesha Microsoft.


”Bill & Melinda Gates Foundation isingelikuwa hivi leo hii pasipo baba yangu,” amesema Gates ambaye baba yake mzazi alikuwa kama mwenyekiti mwenza ilipoanza mwaka 2000.

“Mara kadhaa watu walikuwa wakimuuliza baba yangu kama yeye ndiye alikuwa Bill Gates halisi, ukweli ni kwamba alikuwa kila kitu ninachojaribu kuwa”.

Hata hivyo familia ya Bilionea huyo haijatoa chanzo cha kifo chake, lakini imesema Mzee William Gates II alikuwa dhaifu kiafya.


Bilionea, Bill Gates mwenye umri wa miaka 64, anashika nafasi ya pili duniani kwa watu wenye mkwanja mrefu zaidi, kwa mujibu wa jarida la Forbes Net Worth yake ni dola za Kimarekani Bilioni 98. Wakati tajiri namba moja ni Jeff Bezos ambapo Net Worth yake ni dola Bilioni 113 akiwa na umri wa miaka 56.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad