TMA yatahadharisha upungufu wa chakula nchini



Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, Novemba na Disemba unaonyesha kwamba maeneo mengi ya nchi yatapata mvua chache na hivyo kusababisha athari ikiwemo upungufu wa chakula.

Mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi amesema hayo leo jijini Dar es salaam na kuwashauri wakulima kupanda mbegu za mazao ambazo zinakua hazihitaji maji mengi.


Dkt Kijazi pia ameeleza kuwa athari hizo zitajitokeza si kwa Tanzania pekee bali pia ni kwa nchi zote za Afrika  Mashariki huku akieleza athari hizo kwa sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo wafugaji na wakulima..


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad