Trilioni 7.09 Zitatumika Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR


Na Omary Mngindo, Kisarawe.

SERIKALI kwa mara ha kwanza inatumia zaidi ya shilingi Trilioni 7.09 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, mradi unaoendelea kutekelezwa hapa nchini.

Mradi huo unaolenga kuboresha sekta ya miundombinu kwa ajili ya usafiri na usafirishaji, hivi sasa unaendelea kujengwa kwa kasi, ambao utakapokamilika unakwenda kuwakomboa wasafiri na wasafirishaji wataoutumia usafiri huo.

Hayo yamebainishwa na mgombea Ubunge Jimbo la Kisarawe Alhaj Suleiman Jafo, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni jimboni humo, uliofanyika katika Kijiji cha Kwala Kata ya Chole wilayani hapa.

Jafo ambae ndio Waziri wa TAMISEMI, alisema kuwa sanjali na reli pia kuna ujenzi wa barabara za viwango vya lami zinazounganisha mikoa mbalimbali zinazojengwa kila kona, ikiwa ni hatua ya kuboresha miundombinu hiyo kurahisisha usafiri na usafirishaji.

"Hii haijawahi kutokea, tunajionea juhudi kubwa zinafanyika chini ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, ya kuhakikisha miradi mikubwa inatekelezwa, niwaomba wana-Kisarawe na nchi kwa ujumla kumchagua Magufuli, mimk Mbunge na Madiwani wote.

Alisema kwamba watakuwa wamefanya dhambi kubwa kama hawatutompigia kura nyingi Dkt. John Magufuli, kwani mambo makubwa ameyafanya na anaendelea kuyafanya, huku akiwaomba wana-Kisarawe Oktoba 28 wajitokeze kwa wingi kupiga kura za ndio Magufuli.

Aidha amezungumzia mradi wa barabara ya kiwango cha lami kutokea daraja la Makofia Bagamoyo, Mlandizi Mzenga mpaka Manerumango Kisarawe yenye kilometa 72.9 ambao upembuzi yakinifu umeshafanyika, sanjali na barabara itokayo Uwanja wa ndege mpaka hifadhi ya Nyerere National Park.

Wagombea Ubunge Viti Maalumu mkoani hapa Subira Mgalu, Zaynabu Vulu na Hawa Mchafu waliwaambia wananchi waliojitokeza kuhamikisha wanawapigia kura za ndio wagombea wote wa CCM ili wamalizie kazi walizozianza.

"Mheshimiwa Rais amemuona Jafo anafaa ndio maana amemteua awe msaidizi wake, alipokuja hapa Kisarawe alisema kuwa Jafo anamsaidia kwa kiwango kikubwa, Wizara ya TANISEMI ndio pekee yenye bajeti ya shilingi tririoni 6, natumai atapata kura zaidi ya alizozipata vipindi vilivyopita," alisema Mgalu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad