Trump atuhumiwa kutolipa kodi ya mapato kwa miaka 10



Akiwa anajipanga kwa ajili ya mdahalo wake wa kwanza kabla ya uchaguzi wa Novemba, Rais Donald Trump wa Marekani anakabiliwa na tuhuma mpya za kulipia kodi kidogo ama kutolipia kabisa kwa miaka kadhaa kabla hajaingia madarakani.

 Gazeti la New York Times hapo jana liliibuwa nyaraka zinazoonesha kuwa rais huyo bilionea alilipia dola 750 tu za kodi ya mapato katika mwaka 2016, mwaka alioingia madarakani, na hakulipa kodi yoyote kwa miaka 10 kati ya 15 kabla ya hapo, kwani alidai kupoteza fedha nyingi zaidi kuliko alizokuwa akiingiza kwenye biashara zake. 


Trump, ambaye amezikanusha taarifa hizo akisema ni za uzushi, anajitayarisha kwa mdahalo wa ana kwa ana unaofanyika kesho Jumanne, kati yake na mgombea wa Democratic, Joe Biden. 


Kiongozi huyo wa Republican amevunja mila ya muda mrefu ya marais kuchapisha marejesho yao ya kodi, akiwa amefungua kesi nyingi mahakamani kuzuwia uchapishwaji huo, hali inayochochea uvumi juu ya kile kilichomo ndani yake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad