Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu, ameahidi kuwa iwapo atachagukliwa kuwa rais atahakikisha kila mtanzania anapata bima ya afya ili kuweza kumudu gharama za huduma za afya.
Lissu ameeleza hayo leo Septemba 4, 2020, akiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho mkoa wa Tabora.
“Serikali yetu, serikali ya CHADEMA itahakikisha kwamba, kila mtanzania na kila mkazi wa Tanzania, anapata bima ya afya,” amesema Lissu.
“Ninafahamu, kwa sababau nimepita katika hospitali nlizosema kwa miaka mitano, ninafahamu kwamba bima ya afya ni gharama, uiweka utaratibu wa kila mtu kuwa na bima ya afya, ile gharama ambayo mtalipa kwa mwaka itakuwa ndogo sana,” ameongeza Lissu.