Tundu Lissu Aitaja Tofauti Kati Yake, Mrema na Edward Lowassa

 


Mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu amesema kuwa CHADEMA ya 2020 si kama ile ambayo ilisimamisha wagombea katika uchaguzi kwa miaka iliyopita akiwemo Dkt Slaa na Edward Lowassa kwa kuwa sasa hivi chama hicho kina matawi kila mahali. 


Lissu ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 26, 2020, wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza, na kuongeza kuwa makundi ya watu yanayojitokeza katika kampeni zake hana uhakika kama wote wamejiandikisha kwa sababu huwa hawaulizi.


"Kuna tofauti kubwa kati ya Mrema mwaka 1995, Slaa wa 2010 na Lowassa wa 2015, tofauti kati ya Tundu wa 2020 ni kubwa sana na tofauti yake sasa tuna 'organisation' na ndiyo maana tuko kila mahali kwahiyo tuna uwezo wa kuweka mawakala nchi nzima, uwezo huo hatukuwa nayo miaka ya nyuma, na tuna matawi kila mahali", amesema Tundu Lissu.


Aidha Lissu ameongeza kuwa, "Haya makundi ya watu yanayokuja katika mikutano yetu hatujui kama wanaokuja kwenye mikutano wamejiandikisha kwa sababu hatuwaulizi, katika siasa mtaji ni watu, ukitaka kujua mwanasiasa anaungwa mkono kiasi gani ni watu, ukiona mtu anafanya mkutano wanahudhuria watano ujue huyo hana lolote kwenye ulingo wa siasa".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad