Uchebe Amkataa Shilole ‘Live’

 


Aliyekuwa mume wa mwanamuziki na mjasiriamali maarufu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Ashraf Uchebe amefunguka kumkataa mwanamama huyo.

 

Akizungumzia ishu hiyo miezi kadhaa baada ya kuachana kwao, Uchebe amesema hajui kama anaweza kurudiana na Shilole.

 

“Siwezi kufanya haraka kukurupuka katika uhusiano mwingine na sijui kama naweza kurudiana na Shilole.

 

“Na kuhusiana na yeye kuwa katika uhusiano mpya, sisi wanaume tuna kitu kimoja nikitoka mimi akaingia mtu mwingine, tunakucheka maana tunakuona huna akili.

 

“Mwisho wa siku mimi ninafanya mazoezi ya mwili wangu na kutafuta pesa, sibishani na mapenzi, bali ninafanya kazi na ibada tu,’’ amesema Uchebe ambaye ile kesi yake ya kutuhumiwa kumpiga Shilole, ikiendelea mahakamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad