Uingereza: Daktari huko Gamston hawezi kuchangia damu 'kwakuwa mke wake ni Mwafrika'



Daktari raia wa Kenya nchini Uingereza amesema kuna sheria isiyokuwa na msingi inayomzuia kutochangia damu kwasababu ameoa mke raia wa Kenya

Francis Gĩthae Murĩithi, ametoa wito wa kubadilishwa kwa sheria hiyo ili kutia moyo wachangia wengi zaidi raia wa Waafrika.

Wizara ya Afya Uingereza inasema kwamba ni ''marufuku kwa watu walioa au kufanya mapenzi na mtu ambaye anashukiwa kuwa huenda alishiriki mapenzi na watu wanaoishi nchi zilizoathirika na ugonjwa wa virusi vya ukimwi ikiwemo 'nchi nyingi tu za Afrika' kuchangia damu.''

Kituo cha utoaji damu na upandikizaji Uingereza, kimesema kinaweza kuangalia tena kesi ya Murĩithi.

Daktari Murĩithi, ambaye anafanyakazi kama mtalaamu wa uzazi na maradhi ya kina mama huko East Midlands, alisema yeye na mke wake wa miaka miaka saba walikuwa katika mahusiano ya mume na mke mmoja na hawajawahi kuachana.

Kama daktari, anasema tayari amefanyiwa vipimo tangu alipomuoa mke wake na kwamba hajawahi kupatikana na virusi vya ukimwi.

Lakini anasema aliarifiwa kuwa anaweza tu kuchangia damu ikiwa mke wake pia naye atapimwa virusi vya ukimwi na shirika hilo hilo la utoaji damu au kama watajizuia kushiriki tendo la ndo kwa miezi mitatu.

Murĩithi, 38, ambaye kwa sasa anaishi na Gamston, Nottinghamshire na damu yake ni ile nadra kupatikana ya kundi la AB+, alisema: "Ni sheria isio na msingi inayozuia uchangiaji wa damu.

Ikiwa utafungia watu kama mimi, na uendelee kusema kwamba Waafrika hawajitokezi kuchangia damu, itatufanya tuonekane wabaya wakati ambapo mfumo ndio kizuizi.

"Sitaki nionekane kama msumbufu lakini mfumo wa uchangiaji damu wa Uingereza unahitajika kubadilishwa ili kuruhusu watu wengi zaidi kuweza kuchangia damu.

"Ninafuraha kwamba wanaupitia tena, wanahitajika kupitisha mfumo wa kuangalia mtu mmoja mmoja."

Wizara ya afya Uingereza imekuwa ikitoa wito mara kwa mara kwa watu weusi kujitokeza kwa wingi zaidi na kuchangia damu kwasababu wao ndio wenye uwezekano wa juu wa kuwa na aina nadra sana za damu.


Wizara imesema itakuwa yenye furaha kupitia tena kesi ya daktari Murĩithi hasa kwa kuzingatia kuwa mke wake hana virusi vya ukimwi.

Mshauri wa Wizara ya Afya Uingereza, Su Brailsford, amesema sheria za kuwezesha na kutowezesha uchangiaji wa damu, msingi wake ni ushauri wa kitaalamu uliolenga kupunguza hatari kwa wanaopokea damu hiyo.

Lakini aliongeza: "Tunajua kwamba kutathminiwa kwa hatari zilizopo kwa mtu mmoja mmoja, kunaweza kuruhusu watu wengi zaidi kama daktari Murĩithi kuchangia damu kwa njia salama.

"Tumepanga kupitia upya sera hii ambayo tuna matumaini itaanza kufanyakazi kabla ya mwisho wa mwaka huu."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad