Umoja wa Ulaya wasema Lukashenko sio rais halali wa Belarus



Umoja wa Ulaya umesema hii leo kwamba rais Alexander Lukashenko sio kiongozi halali wa Belarus. Umoja huo umesema hatua ya kuapishwa haraka Lukashenko kuingia madarakani ni kitendo kilichokwenda kinyume na matakwa ya wananchi wa Belarus.

Taarifa ya pamoja ya nchi zote 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya iliyotolewa imebaini kwamba kile kilichoitwa kuapishwa madarakani, na mamlaka mampya yanayodaiwa na Lukashenko yanakosa uhalali wa kidemokrasia wa aina yoyote. 


Taarifa hiyo imekwenda mbali zaidi na kusema kwamba kuapishwa huko kwa Lukashenko kunakwenda kinyume na matakwa ya sehemu kubwa ya idadi ya watu wa Belarus kama ambavyo imejionesha kupitia maandamano makubwa ya umma nchini humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad