Tikiti ni moja ya matunda ambayo hupendwa na watu wengi na yamekuwa na faida zake kiafya, lakini leo naomba tuzifahamu hizi faida za mbegu zake za tunda hilo.
1. Husaidia kulinda afya ya moyo.
Hii ni kutokana na kuwa na madini ya kutosha ya magnesium ndani ya mbegu hizo.
2. Husaidia kwa wenye chunusi
Unapotumia mafuta ya mbegu za tikiti huweza kuwasaidia wale wenye tatizo la chunusi. Ambapo mafuta hayo utapaswa kuyapaka kwa kutumia pamba kwenye sehemu zilizoathirika.
3. Husaidia kuimarisha kinga za mwili
Kutokana na kuwa na madini ya magnesium ya kutosha hiyo husaidia kuimarisha kinga zako za mwili na kufanya kutokumbwa na maradhi mara kwa mara.
4. Huboresha mfumo wa uzazi kwa wanaume
Wanaume wanaotumia mbegu hizi huwa katika hali nzuri kwenye tendo la ndoa na uzalishaji kwa ujumla.
5. Husaidia kuzuia tatizo la nywele kukatika
Mbegu hizi zina utajiri wa fatty acid ambayo husaidia kuboresha afya ya nywele