Urusi na China zatowa mwito kwa Armenia na Azerbaijan kuacha vita



Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imezitolea mwito Armenia na Azerbaijan kujizuia na matumizi ya nguvu kufuatia mapigano kati ya nchi hizo mbili juu ya jimbo lililojitenga la Nagorno-Karabakh. 


Wito huo wa Urusi umetangazwa na shirika la habari la Interfax. wanajeshi wa Armenia na Azerbaijan wamefyetuliana risasi katika mapigano makali katika siku ya pili leo asubuhi ambapo kila upande unamtuhumu mwenzie kwa matumizi ya silaha nzito.


Kadhalika China kupitia wizara yake ya mambo ya nje imesema leo kwamba inataraji nchi hizo mbili zinaweza kuyatatua matatizo yao kupitia mazungumzo na kwamba inataraji zitazingatia utulivu na kujizuia kutumia nguvu.


Msemaji wa wizara hiyo ya China Wang Wenbin amewaambia waandishi habari mjini Beijing kwamba kuendelea kwa amani na uthabiti katika kanda hiyo ni kwa maslahi ya pande zote.


Rais wa Azerbaijan amesaini amri ya kupeleka wanajeshi kufuatia mapigano kwenye eneo hilo la Nagorno-Karabakh.Kadhalika balozi wa Armenia nchini Urusi amesema kwamba Uturuki imepeleka wanajeshi 4000 kutoka kaskazini mwa Syria kuisaidia Azerbaijan


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad