Usifanye kosa hili kwenye mapenzi, utajuta daima. Utageuka kuwa chizi uropoke peke yako barabarani


Najaribu tu kuukumbusha ubongo wako kidogo, jambo dogo ila ndio source ya mambo yote mabaya katika ndoa au mapenzi.

Usiwe na mahusiano ya kimapenzi na mtu unayempenda wewe huku hujajihakikishia kuwa anakupenda pia au la.

Kuwa katika mapenzi na mwanamke au mwanaume anayekupenda na si unayempenda. Ikitokea na wewe umempenda pia itakuwa vizuri zaidi.

Usiuruhusu moyo ukutawale kwenye mapenzi, moyo utakupeleka direct kwa mtu unayempenda bila kujali anakupenda au la na mwisho wa siku utajikuta umeumia.

Kuna nyuzi nyingi za vijana kufanyiwa upumbavu na wapenzi wao humu ndani. Hii inatupa picha kuwa wamependa na hawajapendwa.

Upendo ndio utamfanya mwenzako akuonee huruma na si kukufanya ATM machine kila siku.

Upendo ndio utaleta msamaha toka kwa mwenzi wako pale utakapomkosea.

Upendo ndio utamfanya mwenzako asikucheat hovyohovyo.

Upendo ndio utamfanya mwenzako akusikilize mnapopanga mipango yenu ya kiuchumi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad