Usipime! Liverpool vs Arsenal Kukiwasha Kesho, Jumatatu Ligi Kuu



Msimu mpya wa Premier League umeanza vizuri sana! Baada ya mtanange wa kukata na shoka kuchezwa wikiendi iliyopita, wikiendi hii tunaendelea kunogesha EPL kwa mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal. Anfield patachimbika Jumatatu saa 4 usiku.


 


Je, David Luiz ataweza kumzuia Mohamed Salah? Vipi kuhusu Aubameyang na Lacazatte, wataweza kuisumbua safu ya ulinzi ya Liverpool?


 


Majibu ya maswali haya yanavutia, ukizingatia “The Gunners” wameuanza msimu vizuri zaidi japokuwa timu zote zimeshinda michezo yao miwili ya mwanzo. Arsenal anafaida ya magoli akiwa na tofauti ya magoli 4 ukilinganisha na Liverpool wenye magoli 3.


 


Amini usiamini, wataalamu wa Meridian wameuthamini ushindi wa Arsenal kwa odds ya 6.07. Kama unawaamini vijana wa Arteta, kazi kwako kuwapa ticketi ya ushindi na ujipatie faida kubwa mfukoni mwako!




Mabingwa – Liverpool wamethaminiwa ushindi kwa odds ya 1.52.  Wakati matokeo ya sare yamethaminiwa kwa odds ya 4.21.


Wataalamu wa Meridian wamekuwekea ofa ya machaguo zaidi ya 1,200 ambayo unaweza kuyaangalia hapa.


 


Liverpool walibeba ubingwa msimu ulipita baada ya kupambana kwa miaka 30, hakika Jurgen Klopp anakila sababu ya kuendelea kufurahia mafanikio haya.




Upande wa pili, Arsenal tunaweza kusema walifeli msimu uliopita kwenye Premier League. “The Gunners” walimaliza katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa EPL. Japokuwa, vijana wa Arteta hawakutoka patupu msimu mzima, walibeba Kombe la FA na kuwapa tiketi ya kucheza Europa League msimu huu.


 


Mchezo kati ya Liverpool vs Arsenal unakuwaga ni burudani tupu. Unafahamu kama hii sio mara ya kwanza timu hizi kukutana msimu huu?


 


Arsenal wameshapeleka kilio kwa Liverpool msimu huu baada ya kuwagaragaza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii!


 


Tusubiri tuone kama Arsenal wataweza kurudia/. walichokifanya kwenye ufunguzi wa msimu mpya wa EPL, au kama Liverpool atalipa kisasi?

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad