UTAFITI: Je, unafahamu kuwa, kukaa kwa muda mrefu sehemu moja ni hatari ya kwa afya yako?
0
September 03, 2020
Je, unafahamu kuwa, kukaa kwa muda mrefu mahali pamoja ni hatari ya kwa afya yako? Shirika la Afya Ulimwenguni WHO linakadiria kuwa takribani watu milioni 3.2 kila mwaka hufariki dunia kwa sababu ya kukosa kufanya mazoezi. Tatizo hilo sasa linaukumba ulimwengu mzima.
Misongamano ya magari, kazi za ofisini, kutazama televisheni, kurambaza kwenye mitandao ya intaneti ni baadhi ya mambo ambayo huwafanya watu kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu.
Wanasayansi wanasema kuwa mwili wa mwanadamu uliumbwa kwa sababu ya kutembea ama kusonga, lakini leo, mwanadamu hafanyi mazoezi kama zamani.
Zamani mwanadamu alitembea kwa muda mrefu. Mwanadamu alibeba mizigo. Mwanadamu alishiriki mambo mengi bila ya kutumia mashine na teknolojia.
Daktari Mounir Dia wa Senegal anasema kuwa: “Kuna viungo vingi vya mwilini ambavyo huathiriwa kwa kukosa kufanya mazoezi.” Anaongeza kusema kuwa, “mtu asipoyafanya mazoezi, kuna uwezekano mkubwa wa mapigo ya moyo wake kuongezeka na ni rahisi kupata magonjwa ya moyo.”
Hivyo, mazoezi husaidia kuimarisha mapigo ya moyo na kinyume chake ni kweli, mishipa ya damu huathiriwa, hivyo kuathiri moyo, daktari Dia anasema hali huwa hivyo iwapo mmoja hatafanya mazoezi.
Ujio wa teknlojia na uvumbuzi wa mashine umempunguzia na kumrahisishia mzigo mwanadamu. japokuwa hilo ni jambo zuri kwa upande mwingine, linamuweka mwanadamu kwenye hatari.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, robo ya watu wazima ulimwenguni hawafanyi mazoezi.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, robo ya watu wazima ulimwenguni hawafanyi mazoezi. Kile ambacho hawafahamu ni kuwa kutokufanya mazoezi au kukaa kwa kipindi kirefu ni kujichimbia kaburi.
Inakadiriwa kuwa unapokaa kwa zaidi ya saa nane kwa siku, unastahili kufanya mazoezi ya dakika 60 -75 kila siku, ili kufidia muda uliokuwa umeketi.
Massata ni mfanyabiashara jijini Dakar, mji mkuu wa taifa la Senegal. Anasema kuwa alianza kufanya mazoezi ili kuboresha hali yake ya afya. Uamuzi huo umebadilisha maisha yake. Anasema kuwa, miaka sita iliyopita alikumbwa na ugonjwa. Ugonjwa huo huathiri maini. “Nilikuwa nahisi maumivu mgongoni.” Anasema Massata, huku akiwa ametulia.
Daktari alimfahamisha kufanyiwa uchunguzi kwenye figo zake. Kwa bahati nzuri, matokeo ya uchunguzi yalibainisha kuwa hakuwa na tatizo lolote kwenye figo zake. Kwa bahati mbaya uchunguzi uligundua kuwa alikuwa na mafuta kwenye maini yake.
Aliamua kuanza kuyafanya mazoezi kila siku, baada ya miezi mitatu alirudi kufanyiwa uchunguzi tena. “Uchunguzi wa daktari uligundua kuwa maini yangu yalikuwa yanaanza kurejea kawaida.” Massata ananifahamisha huku akitabasamu.
Anakiri kuwa mazoezi yalimsaidia kupunguza uzito. Mara ya pili aliporudi kuchunguzwa na daktari wake, alifahamishwa kuwa ini lake lilikuwa sawa kabisa bila ya matatizo.
mabadiliko ya tabia ya kula pamoja na mazoezi ya mara kwa mara ni dawa mjaarabu kwa mujibu wa matabibu.
Ugonjwa aliokuwa akiugua ni kuwa ini huzungukwa na mafuta. Mara nyingi watu wenye ugonjwa huo, huwa hawaoneshi dalili zozote.
Hadi kufikia sasa hakuna dawa au matibabu ambayo yamethibitishwa kuponya ugonjwa wenyewe. Hata hivyo mabadiliko ya tabia ya kula pamoja na mazoezi ya mara kwa mara ni dawa mjaarabu kwa mujibu wa matabibu.
“Kabla nianze kufanya mazoezi, nilikuwa na uzani wa kilo 86, lakini sasa uzani wangu ni kilo 76. Mazoezi yalinasaidia kupoteza kilo 10 kwa kipindi cha miezi mitatu.” Massata anasema huku akionekana akiridhishwa na hali yake sasa.
Anaafiki kuwa mazoezi yana nafasi kubwa sana maishani mwake sasa. Zamani hakuwa na muda alioutenga kwa ajili ya mazoezi lakini sasa anasema, “mimi hufanya mazoezi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Shirika la Afya Ulimwenguni linapendekeza mazoezi ya dakika 30 kwa watu wazima na saa moja kwa watoto
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Tangu agundue umuhimu wa kufanya mazoezi, Massata, hajawahi kuwa mvivu katika maisha mapya aliyoanza kuyaishi. “Hapa huwa ninakuja kufanya mazoezi kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, isipokuwa mwishoni mwa juma. Misuli inahitaji kupumzika ili ikue.” Massata ananifahamisha huku akiwa kwenye eneo ambalo hufanyia mazoezi akiwa na nguo za mazoezi.
Baada ya mazungumzo, mara Massata ananifahamisha kuwa kocha wake kwa jina Lamine ndiye mwokozi wake. Bila Lamine hali yake ingekuwa mbaya mno. “Nazungumzia umuhimu wa kuwa na mahusiano mema.” Massata ananifahamisha kisha anamuita kocha wake.
Kisha kocha wake anafika huku akiwa mwingi wa tabasamu, “wakati mwingine sikumuona akija kufanya mazoezi. Ukweli ni kuwa alikuwa anatibiwa hospitalini. Aliporejea mazoezini aliniambia alikuwa ana furaha kubwa.” Lamine anasema, kisha anaendelea kuzungumza, “nilimuuliza, nini kilichofanyika?”
Massata alimkumbatia na kumfahamisha kuwa, amepona. Amepona kwa ukamilifu.
Shirika la Afya Ulimwenguni linapendekeza mazoezi ya dakika 30 kwa watu wazima na saa moja kwa watoto. Bila hivyo, inachukuliwa kuwa hufanyi mazoezi.
Hata hivyo daktari Dia anasema kuwa mazoezi ya kila siku humsaidia mtu kufidia muda ambao alikuwa ameketi kwa kipindi kirefu.
kufanya mazoezi ni kuokoa muda ama wakati. Kufanya hivyo kunaondoa uchovu na unahisi mwenye nguvu haswa unapoamka.
Anashauri kuwa ni muhimu kupunguza muda ambao mtu huketi. Anasema kuwa mtu hafai kuketi kwa zaidi ya saa tatu. Anaongeza kusema kuwa, kwa wale wanaofanya kazi ofisini wanastahili kuinuka kila wakati, kutembeatembea kabla ya kurejea kwenye viti vyao.
Daktari Dia anasema kuwa kuketi kwa muda mrefu huathiri mwendo wa damu. “Kile ambacho mara nyingi husingizia kwa kutofanya mazoezi ni muda ama wakati. Hata hivyo, ni muhimu kutenga muda wa kufanya mazoezi ili usihatarishe maisha yako.” Anamaliza kueleza.
Ama kwa hakika, kufanya mazoezi ni kuokoa muda ama wakati. Kufanya hivyo kunaondoa uchovu na unahisi mwenye nguvu haswa unapoamka.
Mtindo wa maisha wa kukaa tu, unachangia asilimia 30 ya maradhi ya moyo na kati ya asilimia 20-25 ya saratani ya matiti kibofu na mapafu.
Wataalamu wanasema kuwa iwapo umezoea kushinda kwenye kiti kazini kwa kipindi kirefu, yafuatayo ni mambo ambayo unaweza ukayafanya:
-Iwapo unashuka kwenye basi hakikisha kuwa unashuka mbali na ofisi ili upate nafasi ya kutembea.
-Iwapo unaendesha gari, hakikisha unaliegesha mbali na kiasi na mahali pa kazi, ambapo utatembea.
-Badala ya kutumia kambarao/lifti, hakikisha unatumia vidato.
– Simama kwa dakika moja, kila baada ya saa moja ama dakika tano hadi 10 kwa
kila dakika 90
Tags