Wafanyakazi wa hoteli wavuliwa nguo kwa shutuma za wizi Nigeria



Kundi la wakili wa haki za binadamu mjini Warri, kusini mwa Nigeria, linatafuta fidia ya kuwalipa wafanyakazi wanne ambao walidaiwa kuvuliwa nguo na mwajiri wao.

Wafanyakazi hao wanashutumia kuiba fedha za wageni, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti baada ya kuambiwa na baadhi ya wageni.

Wafanyakazi hao walikuwa wanne, watatu wakiwa wanawake na mmoja mwanaume waliamuriwa kuvua nguo na kuvua nguo huku polisi wakiwa wanashuhudia.

Picha na video za wahanga hao wakiwa wamesimama bila nguo zilitumwa na wengi mtandaoni.

Wakili wamemuandikia barua mmiliki wa hoteli ambaye ni waziri wa zamani wa Nigeria kwa kuvunja sheria kwa udhalilishaji na kuingilia faragha ya wengine.

Wakili hao wanamtaka aombe radhi umma pamoja na kulipa fidia kwa wafanyakazi aliowadhalilisha.

Waliofanyiwa vitendo wanadai picha zilizorushwa mtandaoni zilikuwa zinawadhalilisha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad