Wafungwa saba kati ya 219 waliotoroka gerezani Uganda wakamatwa

 


Wafungwa saba kati ya 219 waliotoroka kutoka katika gereza kaskazini-mashariki mwa Uganda wamekamatwa. Wafungwa hao walimpiga risasi na kumuua askazi ambaye alijaribu kuwazuwia kutoroka, kabla ya kukimbilia kwenye mlima wa Moroto-Mount Moroto Jumatano mchana.

 

Msemaji wa hudma za magereza nchini humo amesema wamepeleka helikopta tatu na askari wanaotembea kwa miguu kuwasaka wafungwa hao. Wawili kati yao wamepigwa risasi na kufa.

 

Inasemekana wafungwa hao walitoroka na bunduki 15 pamoja na risasi.


Jengo la gereza hilo liko kwenye eneo la mlima Moroto- Mount Moroto, pembeni mwa mji huo.


Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, wafungwa walivua sare zao za jela za rangi ya manjano na kukimbia uchi milimani kuepuka kubainika.


Inaaminia kuwa wafungwa hao walikuwa wakijaribu kutumia njia ya milimani kuvuka ili waweze kuvuka mpaka waingie Kenya


Gereza hilo ambao kwa kawaida huwahifadhi wafungwa 600, kwa sasa limefungwa huku uchunguzi ukiendelea kubaini ni vipi wafungwa hao walivunja gereza na kutoroka.


Jeshi limetuma picha ya msako wao dhidi ya wafungwa:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad